Mtandao wa Rafiki

Ndani ya timu ya GCS ni jeshi la watu wanaouza nyumba kwa nyumba,kwenye magulio au kwa mitandao binafsi.Wachezaji hawa tunawaita Rafiki.Rafiki hawa ndio uti wa mgongo wa GCS na viongozi katika jamii zao.

Jiunga timu ya Rafiki sasa!

*** Candidates must be Tanzanian citizens

Tunataka kuwatambulisha wawili kati ya Rafiki hao waliosambaa nchi nzima, Lelu Sailepu na Lilian Mpongoliana.


Lelu Sailepu

Lelu 2

Kijiji: Aracatan

Kabila: Maasai kutoka mkoani Arusha

Kaanza tokea: 2012

Idadi ya bidhaa alizouza tokea mwaka 2012: 417

Wastani wa ongezeko la mapato kutokana na mauzo ya  GCS : 100,000 TSH kila mwezi kutokana na faida

Ni kwa kiasi gani kuwa  rafiki  wa GSC kumekuza kipato chako?: Ukilinganisha na maisha yangu kabla ya GCS, Nilikuwa nahangaika kila siku kuitunza familia yangu kwa vile sikuweza kupata kazi ya uhakika. SASA nina kipato cha uhakika na najiskia vizuri kuweza kuitunza familia yangu .Tuna chakula mezani  kila siku na nina uhakika na chakula cha kesho